(1) SHETANI NI MJARIBU
katika Math 4:3 neno la Mungu linasema "Mjaribu akamjia" Mjaribu anayetajwa hapo si mwingine isipokuwa ni shetani/ibilisi kama tutakavyozidi kuona mbeleni kidogo. Hapa tunaona Yesu Kristo Mwana wa Mungu kabla ya kuanza kuombea watu, kufundisha na mengineyo baada tu ya kubatizwa kilichofuata ni Yesu Kristo kupandishw
a nyikani ili ajaribiwe na ibilisi.
Ilikuwa lazima ajaribiwe kwa sababu shetani hana jipya yale yote aliyomjaribu Yesu ndio nguvu zake zote, ushawishi wake wote, mbinu zake zote alizitumia hapo, maana yake tukitaka kumjua vizuri shetani na kazi zake tunazipatia hapo maana alijua anakutana na Mwana wa Mungu hivyo nguvu, ushawishi, mbinu alizozitumia hazikuwa ndogo.
Katika maisha yetu ya kila siku tunakutana na majaribu ambayo chanzo chake ni shetani, majaribu yote yanabeba uwakilishi wa shetani zidi yetu. Viwango vyetu sisi wanadamu wakati mwingine kwa huruma za Mungu huenda asimruhusu shetani aje kwetu mzima mzima isipokuwa wawakilishi wake ambao wanabeba kusudi lile la bosi mkuu wao. Lakini kila kukicha tunakutana na majaribu ambayo lengo lake ni kuhakikisha hakuna mwanadamu yeyote ambaye anaweza kumuona Mungu.juu
(2) KUACHIWA KWA MAJARIBU KATIKA MAISHA YETU
Mwanzoni kabisa tunaona Yesu anapelekwa na Roho nyikani ili ajaribiwe Math 4:1 "Kisha Yesu akapandishwa na Roho nyikani ili ajaribiwe na ibilisi". Anapelekwa na Mungu katika kujaribiwa sio kwamba amefanya dhambi yo-yote hapa, ila hakuna namna yoyote ya kutenganisha majaribu na imani yetu. Ndio maana kabla ya yote mengine kuanza katika huduma ya Yesu ili lazimu ajaribiwe. Huwezi kutenganisha imani ya Ukristo bila majaribu hilo haliwezekani.
Mtu anapoamua kumuamini Yesu tayari lazima mjaribu aje kutujaribu hilo ni lazima. Mungu anayaachia majaribu, mitihani ili kujua kuwa tunampenda Yeye kwa kiasi gani lakini upande wa pili shetani ana mawazo tofauti na sisi, yeye lengo lake ni kutuua kabisa yaani kutumaliza.
Mungu haachii hayo ili kutukomoa, kutudhalilisha, kutufedhehesha hapana. Hapana! Mungu upendo wake kwetu uko juu mno kupita vile tunavyoweza kuwaza.
Nazungumza na mtu ambaye wakati huu yupo katika mapito makali sana, inafikia mahali unatamani kujiua, kuacha huduma, kurudi nyuma kwa sababu ya hayo unayoyapitia! Majaribu ni sehemu ya mwanafunzi.
(3) WAKATI WA NJAA
Ibilisi/Shetani huja wakati tunapopita katika vipindi vya njaa, vipindi ambavyo tunapitia maisha magumu kwa kiwango ambacho hata pesa ya kununua chakula tunakosa. Kipindi hiki shetani huwa hachezi mbali na mtu wa namna hiyo, atakuwa karibu mno!
Alipogundua Yesu ana njaa alimwambia aamuru mawe yawe mikate ili ale chakula. Alimwambia Yesu aamuru mawe yawe mikate kwa sababu aliujua uwezo wake mkuu! Lakini akija kwetu atatumia wakati huo kuhakikisha anatuambia jambo lolote la kutaka kujaribu kutuamrisha ili tuone kipindi cha njaa tunachopitia ni kipindi ambacho si sahihi kwetu.
Anaweza akatuambia MUNGU wako unayemuamini yuko wapi? Anaweza kutumia majirani, marafiki, mke, mume, watoto na wengineo. Watakuuliza Yesu wako yuko wapi unayemuamini mpaka anakuacha unalala na njaa!
Njaa ilimfanya Esau kuuza uzaliwa wake wa kwanza ( Mwa 25:29-34). Njaa inaweza kabisa kutufanya kumuacha Yesu, au kuiacha imani tuliyoipokea kwa kufanya mambo yasiyompendeza Munguu
(4) KUUA, KUCHINJA, KUHARIBU
Shetani ana kazi tatu tu, KUIBA, KUCHINJA NA KUHARIBU (Yoh 10:10)
Kila analolileta linakuwa kwenye kundi moja kati ya hayo matatu. Lakini makusudi yake ni kuhakikisha mtu anarudi nyuma kwa kumuacha BWANA!
Shetani siku moja alizungumza na Mungu, Mungu akamuuliza shetani umetoka wapi? Shetani akajibu nimetoka kuzunguka - zunguka. Mungu akamwambia umemuona Mtumishi wangu Ayubu? Mjaribu akaomba nafasi ya kufanya kazi zake tatu yaani kuiba, kuchinja na kuharibu. (AYUBU 1:6-12)
Shetani alianza na kuua watoto kumi wa Ayubu, na mambo mengine yote mabaya yakampata Ayubu kwa mpigo mali zake zote ziliteketezwa, akaumwa magonjwa yasiyoponyeka kwa mateso makali mno. (AY 1:13-22)
Shetani akipata nafasi huitumia kisawasawa; lakini maandiko yanatuambia katika AYUBH 1:22 "Katika mambo hayo yote, Ayubu hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu". Hayo ndio yalikuwa malengo ya shetani yaani Ayubu afanye dhambi aanze kunung'unika na kumuwazia Mungu kwa upumbavu lakini Ayubu alishinda.
Ndivyo ilivyo na kwetu, haya ambayo tunakutana shetani anataka tufanye dhambi, tumuwazie MUNGU kwa upumbavu. Sisi tunatakiwa kuwa kama Ayubu uendelee kumuamini Mungu.
Mwisho wa Ayubu ulikuwa mzuri sana (AYUBU (42:10-17) Na sisi mwisho wetu utakuwa mzuri sana kama tukiendelea kumng'ang'ania BWANA.
(5) JINSI YA KUMSHINDA SHETANI/IBILISI KATIKA MAJARIBU YETU
(A) MANENO YA MUNGU YAJAE MIOYONI MWETU
Yesu Kristo wakati anajaribiwa alikuwa anajibu imeandikwa hakuwa anafanya miujiza yo-yote kwa shetani isipokuwa alikuwa ana jibu kwa kutumia maandiko.Hakuna namna yo-yote nyingine ya kumshinda shetani kama hatutaki maneno ya Mungu yakae vinywani mwetu hakuna! Lazima tuwe na vipindi vya kusoma Neno la Mungu wenyewe, pia kujifunza kutoka kwa wengine kinachotakiwa ni maneno ya Mungu yakae kwa wingi ndani. (ZAB 119:11, MATH 4:3-11)
Tuwe makini sana na muda wetu, tuwe wasomaji wa Biblia kila siku.
(B) MAOMBI
Lazima tuwe na vipindi vya maombi tena kila siku kiwango cha chini ni saa moja tu! (MATH 26:41) "Kesheni muombe msije mkaingia majaribuni".
Tukiwa na maisha ya maombi majaribu yakija tutaweza kuyashinda kiwepesi na kirahisi, hatutoshindwa hata kidogo hata kama ubinadamu utakuwepo, maumivu, machungu lakini mwisho wake ni kushinda..lakini wakati mwingine maombi hutujaza amani kubwa mioyoni mwetu, amani kubwa mno.
conquerorintheuniverse@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni